Yesu ni
nani?
Watume wa Agano La kale wanatueleza kuhusu kuja kwa
Massia
Isaya
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto
mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye
ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, baba
wa milele, Mfalme wa amani. Isaya 9:6
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira
atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina
lake Imanueli-maana yake Mungu pamoja nasi. Isaya 7:14
na Mathayo 1:22-23
Danieli
Nikaona katika njozi za usiku na tazama, mmoja aliye mfano wa
mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo
mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na
utukufu na ufalme, ili watu wa kabila zote na taifa zote na
lugha zote wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele,
amabayo hayatapita kamwe na ufalme wake ni ufalme usioweza
kuangamizwa. Danieli 7:13-14.
Katika
Agano Jipya
Mwana wa Mungu
Akawaambia, “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?” Simoni Petro
akajibu akasema, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye
hai.” Yesu akajibu, “akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona;
kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hiliu, bali Baba yangu
aliye mbinguni.” Mathayo 16:15-17.
Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda
kazi. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua,
kwa kuwa hakuivunja sabato tu,bali pamoja na hayo alimwita
Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Yohana
5:17-18
Yesu akajibu; “Mimi na Baba tu umoja.” Basi Wayahudi
wakaokota mawe tena ili wampige, lakini Yesu akawajibu, Kazi
njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya
kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu,
“Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda,” bali ni
kuwa umekufuru. “Wewe ingawa ni mwanadamu unajufanya kuwa
Mungu.’’ Yohana 10:30-33
Baada ya kukamatwa na kutiwa nguvuni, viongozi wa Wayahudi
wakauliza; “Wewe basi ndiye Mwana wa Mungu?” Yeye akawajibu,
“Ninyi mmesema kwamba Mimi ndiye.’’ Luka 22:70
Aliyefufuka
Ingawa milango zilikuwa zimefunguwa, Yesu alikuja na kusimama
katikati yao na kusema, “Amani iwe nanyi’’. Kisha akamwambia
Thomasi “Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyosha
mkono wako uguse ubavuni Mwangu. Usiwe na shaka bali uamini
tu.” Thomasi akamwambia, “Bwana wangu na Mungu Wangu!” Yesu
akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale
ambao hawajaona lakini wameamini.’’ Yohana 20:26-29
Nikamwona mtu kama, “Mwana wa Adamu’’ amevaa joho refu na
mkanda wa dhahabu umefungwa kifuani mwake. Kichwa chake na
nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji,
nayo macho yake yalikuwa kama mwali wa moto. Nyayo zake
zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama vile imesafishwa
katika tanuru ya moto, nayo sauti yake ilikuwa kama sauti ya
amji mengi. Katika mkono wake wa kuume alishikilia nyota saba
na kinywani mwake ulitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake
kama jua kali linalong’aa kwa nguvu zake zote.
Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama aliyekufa. Ndipo
akaweka mkono wake wa kuume juu yangu na kusema, “Usiogope,
Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho. Mimi ni yeye aliye hai,
niliyekuwa mimekufa na tazama ni hai milele na milele! Nami
ninazo funguo za mauti na za kuzimu.” Ufunuo wa Yohana 1:13-18
Unaweza pata uhai kwa Jina lake
Yesu alifanya miujiza mingine mingi mbele ya wanafunzi wengi
Wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. Lakini haya
yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo Mwana
wa Mungu na kwa kumwamini mpate uzima katika Jina Lake.
Yohana 20:30-31
Moyo
wa ujumbe wa Biblia
Hadithi ambozo zifuatozo kukamata moyo wa ujumbe wa Biblia
kwa njia mpya.
1. Dereva
Dereva mmoja alisimamishwa na afisa wa polisi. Alikuwa dereva
stadi na kwa mujibu wa ufahamu wake hakuwa amekiuka sheria za
trafiki.
Afisa wa polisi akasema, “nilikuweka kando kwa sababu ulikuwa
ukiendesha gari kwa kiasi ya kilomita 55 kwa saa katika eneo
la shule. Palikuwa na tangazo ya sheria kumi za kutahadharisha
kuwa kiasi ya juu inayokubaliwa ni kilomita 15 kwa saa lakini
ulizipuuza zote.”
Kwa vile dereva huyo alivyokuwa na ishara kumi za kumuonya,
Mungu ametupa ishara kumi zilizo wazi za tahathari katika
Bibilia. Zinajulikana kama Amri Kumi.
Je, umewahi kusema uongo, kuiba kitu au kutumia jina la Mungu
kwa mzaha? Ikiwa u kama mimi, jawabu ni ndio.
Sikiliza Bibilia inavyosema:
Yeyote awekaye sheria yote lakini anajikwaa kwa moja amevunja
yote. Jakobo
2:10
Mungu anasema kuwa kuivunja amri moja tumefanya dhambi na
tutatakiwa kutoa hesabu kwa kuvunja amri zote, hata ile ya
usinzi na uuwaji.
Hukumu ya Mungu kwa dhambi zetu ni kifo. (kutupwa jehanamu
kwa sababu hatakubalia dhambi mbele ya uwepo wake).
Warumi
6:23a
Kama hadithi hii ikiishia hapa, hakuna tumaini kwetu…
2. Mhukumiwa
Mtu aliyekuwa na hatia alimuendea hakimu na kujitolea kuuawa
kwa niaba ya muuaji aliyapatikana na hatia. Hakimu alikubali.
Siku iliyofuata hakimu alimuambia mhukumiwa kuwa alikuwa na
uamuzi wa kufanya.
“Mtu asiye na hatia ameuawa badala yako. Ikiwa utakubali
fidia yake kwa kosa lako, una uhuru wa kuenda.
Ikiwa hutakubali fidia yake, utauawa kwa kosa lako. Umechagua
lipi?”
Yesu Kristo, Mwana wa Mungu ingawa hakuwa na dhambi, aliutoa
uhai wake kwa hiari ili kulipia adhabu zako na zangu. (Hukumu
ya Mungu kwa dhambi zetu ni mauti). Siku tatu baadaye
alifufuka kutoka kwa wafu.
Mungu alidhihirisha upendo wake mkuu kwetu kwa kumtuma Yesu
ili afe kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Warumi 5:8
Kipawa cha Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana
wetu. Warumi 6:23b
Kutokana na kifo cha Yesu kwa niaba yako, una maamuzi mawili:
Pokea msamaha wa Mungu kwa dhambi zako pamoja na uzima
wa milele kwa kutubu (kutambua hali yako ya dhambi na kutamani
kutoka katika hali hiyo) na kuweka tumaini lako katika Bwana
Yesu. (Matendo ya Mitume 20:21)
Au
Kukataa msamaha wa Mungu kwa dhambi zako pamoja na
uzima wa milele kwa kumtumaini yeyote au chochote ila Yesu ili
akufanye au kikufanye ukubalike kwa Mungu. Hivyo basi wewe
mwenyewe ubebe adhabu kwa kuvunja sheria.
Kwa vyovyote vile wanaoamini katika mwana wana uzima wa
milele, lakini yeyote anayemkataa Mwana wa Mungu hatauona
uzima, kwa kuwa ghadhabu ya Mungu imekaa juu yake.
Yohana 3:36
Kujua kuhusu Yesu hakumaanishi unamuamini...
3. Mruka Angani
Waruka angani hudhihirisha imani yao katika miamvuli
wanapovuka kutoka kwa ndege.
Wafuasi wa Yesu hudhihirisha imani yao kwake Roho wa Mungu
anapowabadilisha katika mawazo na shauku zao.
Yeyote aliye katika Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale
yameisha, na yamekuwa mapya! 2 Wakorintho 5:7
Mungu asema, “Nitawapa moyo
mpya na kuweka roho mpya ndani yenu.” Ezekieli
36:26
Kama vile kuingia katika kiwanda hakuwezi kukufanya kuwa
fundi wa magari, kuhudhuria kanisani hakutakufanya Mkristo.
Ikiwa ungependa kuupokea msamaha wa Mungu kwa dhambi zako na
kipawa cha uzima wa milele, tafakari kuhusu kufanya ombi
lifuatalo:
“Yesu, naamini ulilipa adhabu ya dhambi zangu ulipokufa
msalabani na kufufuka kutoka kwa wafu. Nataka kugeuka kutoka
kwa dhambi zangu na kuweka tumaini langu kwa Bwana wangu.
Nataka kukufuata katika maisha yangu yaliyobaki. Amina.”
Yeyote anayeliitia jina la Bwana ataokoka. Warumi
10:13
Wafuasi halisi wa Yesu huwa na shauku ya:
Kuishi maisha yanayolingana na uungu, kupendeza Mungu kwa
njia zote, kuzaa matunda katika kazi zote vyema na kukua
katika kumjua Mungu. Wakolosai 1:10
http://www.tracts.com/Kiswahili.html